Loading...

Chelsea wamepewa nafasi ya kumsajili nyota huyu wa Klabu ya Juventus


'The Blues' wanatarajiwa kufanya usajili wa kushitukiza kwa Dan Alves. Inaripotiwa kwamba, Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uingereza sasa wanafanya mchakato kufuatia kupewa taarifa ya uwepo wa beki wa kulia wa Juventus, Dan Alves.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34, anatarajiwa kuwa kwenye kikosi kitakachoivaa Real Madrid kwenye fainali ya UEFA, hata hivyo, 'future' yake pale Torino ni ya mashaka.

Mtandao wa Daily Mail unatoa ripoti zinazodai kwamba 'The Blues' wamepewa nafasi ya kumsajili nyota huyo kutoka taifa la Brazil na Antonio Conte inaonesha yuko tayari kumsajili nyota huyo wa zamani wa Barcelona.

Conte ana mipango mikubwa kwa kikosi chake kuelekea msimu ujao kwenye Ligi ya Mabingwa ya Ulaya (UEFA) na kumtafutia Victor Moses mapinnzani katika nafasi ya 'full beki' ya kulia ikiwa ni eneo mojawapo ambalo Menaja huyo wa Chelsea ana mpango wa kuliongezea nguvu

Hata hivyo, 'The Blues' watakumbana na upinzani kutoka kwa mahasimu wao wa Uingereza, Manchester City na Tottenham kwa sababu klabu zote hizo nazo zilikuwa kwenye mchakato wa kuisaka saini ya Alves.

Alves alitimiza miaka 34 mwezi uliopita na bado amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Mabingwa wa Ligi ya Sirie A, Juventus.
Chelsea wamepewa nafasi ya kumsajili nyota huyu wa Klabu ya Juventus Chelsea wamepewa nafasi ya kumsajili nyota huyu wa Klabu ya Juventus Reviewed by Zero Degree on 6/03/2017 07:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.