Loading...

Conte amemtaja mchezaji anayeweza kuziba pengo la John Terry

Leonardo Bonucci akiwa na Kocha wake, Antonio Conte Timu ya Taifa Italia
Kwa mujibu wa ripoti, Antonio Conte hana shaka ana uwezo wa kumsajili Leonardo Bonucci kuziba pengo la John Terry.


Ripoti zinadai kwamba, wakati Real Madrid, Manchester City na Manchester United wote wameelekeza macho yao kwa Bonucci, Conte inawezekana akawa ndio mwenye nafasi kubwa ya kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 kwani amewahi kuwa Mkufunzi wake alipokuwa Juventus na katika Timu ya Taifa ya Italia.

Beki huyo wa Italia ameitumikia Juventus vilivyo katika msimu huu, akitoa mchango wake pia kusiadia timu yake kufika hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo imechezwa wiki iliyopita.

Inaonekana Chelsea watokea kuipenda kazi ya Bonucci baada ya kumtazama msimu huu, kama wanavyozidisha juhudi za kuboresha safu yao ya ulinzi kuelekea mashindano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Na ripoti zinadai kwamba Antonio Conte amemtaja Bonucci kama chaguo sahihi la kuziba pengo la John Terry.

Ripoti za Mitandao zinaendelea kwa kusema kwamba, Chelsea wako tayari kumpa beki huyo mshahara wa pauni laki moja na elfu kumi na tano (
£115,000) kwa wiki.
Conte amemtaja mchezaji anayeweza kuziba pengo la John Terry Conte amemtaja mchezaji anayeweza kuziba pengo la John Terry Reviewed by Zero Degree on 6/06/2017 08:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.