Loading...

Vifo vya paka vyazua hofu nchini Ufaransa


Kijiji kimoja cha starehe kilicho kusini mwa Ufaransa kimekumbwa na wasi wasi baada ya zaidi ya paka 200 wa kurandaranda na wa kufugwa kufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kula sumu.

Kisa hicho kimetokea eneo la Saint Pierre la Mer kilomita 90 kutoka Kusini magharibi mwa Montpellier.

Chama cha kuwalinda wanyama kimepokea simu nyingi kufuatia kisa hicho.

Wanyama wengine na hata ndege nao walikufa baada ya kula sumu, huku kukiwa na hofu kuwa watoto huenda nao wakaila.

Chama cha paka wa kurandaranda kimeripoti matukio hayo kwa polisi kwa matumaini kuwa uchunguzi utafanywa.

"Tuna hofu kuwa mtota anawewa kuila sumu hii," mwanakijiji mmoja mwenye hofu alisema.
Vifo vya paka vyazua hofu nchini Ufaransa Vifo vya paka vyazua hofu nchini Ufaransa Reviewed by Zero Degree on 6/06/2017 08:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.