Loading...

Conte atabakia Chelsea hadi mwaka 2021, imeripotiwa!


Mashabiki wa Chelsea wanaendelea kusambaza Habari njema baada ya kuwekwa hadharani habari za kwamba, Antonio Conte anakaribia kusaini mkataba mpya na 'The Blues'.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Italia, Conte atasaini mkataba mpya utakaomfanya awe meneja wa Chelsea hadi mwaka 2021 huku mkataba huo ukimwingizia kati ya paundi milioni 9.5 hadi 10 kwa mwaka, na kumfanya kuwa kocha anayelipwa fedha nyingi katika historia ya klabu.


Muitaliano huyo bado amesalia na miaka miwili katika mkataba wake wa sasa lakini klabu wanahitaji kumbakiza pale Stamford Bridge hasa baada ya kuisaidia Chelsea kutwaa ubingwa wa LIgi Kuu katika msimu wake wa kwanza.

Inasemekana Conte amefanya mazungumzo na mkurugenzi wa klabu, Marina Granovskaia siku ya jumapili na alikuwa na furaha kwa mazungumzo yao juu ya mkataba wake na mipango ya klabu kwa majira haya ya joto.

Habari hii inakuja ikiwa imepita wiki moja tu baada ya kusambaa kwa tetesi zilizodai Conte yuko kwenye harakati za kuondoka Chelsea baada ya kukerwa na utaratibu wa shughuli nzima ya usajili kuelekea msimu ujao.
Conte atabakia Chelsea hadi mwaka 2021, imeripotiwa! Conte atabakia Chelsea hadi mwaka 2021, imeripotiwa! Reviewed by Zero Degree on 6/22/2017 05:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.