Singida United yamsajili beki wa zamani wa Simba SC
Mratibu wa Singida United, Festo Sanga, alisema kuwa Miraji ambaye msimu uliopita aliichezea African Lyon kwa mkopo amesaini mkataba wa miaka miwili.
Sanga alisema kuwa wanaamini mchezaji huyo ataongeza nguvu katika kikosi hicho na hatimaye kiweze kufanya vizuri katika mechi za msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kushindana na klabu nyingine zenye uzoefu katika ligi hiyo ya juu hapa nchini.
Alisema kuwa baada ya kufikia makubaliano na beki huyo, tayari wamempa jezi namba nne na atafuata kanuni na masharti yote ambayo yametajwa kwenye mkataba wake.
Aliongeza kuwa mbali na kusajili nyota wengine kutoka ndani na nje ya nchi, bado mchakato wa usajili wa wachezaji haujamalizika na viongozi wamejipanga kutekeleza mahitaji yote yaliyoelekezwa na benchi la ufundi.
Sanga alisema kuwa wanaamini mchezaji huyo ataongeza nguvu katika kikosi hicho na hatimaye kiweze kufanya vizuri katika mechi za msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kushindana na klabu nyingine zenye uzoefu katika ligi hiyo ya juu hapa nchini.
"Tunafurahi kumtangaza Miraji Adam kuwa ni mchezaji wetu mpya, ameungana katika familia ya Singida United, ni mchezaji ambaye amesajiliwa kwa kufuata mapendekezo yaliyotolewa na kocha wetu," alisema Sanga.
Alisema kuwa baada ya kufikia makubaliano na beki huyo, tayari wamempa jezi namba nne na atafuata kanuni na masharti yote ambayo yametajwa kwenye mkataba wake.
"Jumla sasa tumesajili wachezaji wapya wa nje sita na wandani wanne, tunatarajia kuanza mazoezi ifikapo Julai Mosi, kocha wetu mkuu atakuwa amerudi kwa ajili ya kusimamia programu yake ya ufundi," alisema mratibu huyo.
Singida United yamsajili beki wa zamani wa Simba SC
Reviewed by Zero Degree
on
6/22/2017 03:03:00 PM
Rating: