Loading...

Eric Cantona amemkosoa Conte kwa kitendo hiki alichofanya


Eric Cantona amejitokeza na kumkosoa meneja wa Chelsea, Antonio Conte kwa kitendo alichomfanyia Diego Costa.

Wiki mbili zilizopita, Conte alimweleza Costa kwa kupitia ujumbe wa simu kwamba hana nafasi katika mipango yake ya msimu ujao.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye amekuwa na uhusiano wa mashaka na Conte kwa msimu uliopita, yuko katika wakati usioelezeka kuhusiana na maisha yake yajayo ya soka kufuatia tukio hilo. Na mwenyewe anaendelea kutafuta klabu nyingine ya kuhamia kwa msimu ujao.

Mkongwe wa Manchester United, Cantona ana amini Conte ana makosa kwa kumuacha Costa katika mazingira yale na ana amini kitendo hicho kinaweza kuisababishia madhara Chelsea kwa baadaye.


Cantona alisema: “Meseji za hasira, sio wazo zuri kabisa na ni njia mbaya zaidi ya kumalizana na mtu.

“Weka wote pamoja na utaona umaarufu wa Conte umeshuka sasa: ‘Nakutakia maisha mema kwa mwaka ujao lakini hauko katika mipango yangu.’

“Kila neno moja la sentensi hiyo iliyotumwa kwa Costa linaweza kuigharimu Chelsea kiasi cha euro milioni 1.

“Usiiongoze timu kwa kutumia kidole gumba!”
Eric Cantona amemkosoa Conte kwa kitendo hiki alichofanya Eric Cantona amemkosoa Conte kwa kitendo hiki alichofanya Reviewed by Zero Degree on 6/18/2017 05:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.