Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 05
MTUNZI: MC Short Charles Gwimo
Ilipoishia..........Kwa kuwa jamaa yangu alikuwa ni mdadisi, hakusita kunidadisi kuhusu kutokuwa na furaha asubuhi hiyo. Nilimuoneshea tabasamu feki ili nimridhishe kuwa niko sawa lakini hakuonekana kuukubali usemi wangu hivyo akaendelea kunibana ili nimueleze yaliyonisibu. Kwa kuwa urafiki huzidi mwanasesere niliona isiwe kesi bali nimueleze yaliyonisibu ila kwa uongo zaidi. Nilimdanganya kuwa usiku huo nilipata kuota njozi mbaya ambayo niliona nimezungukwa na wachawi wakitaka waninyonye damu na kunifanya kitoweo nikawakemea kwa mujibu wa imani yangu wakatoweka ghafla. Rafiki yangu alinipa pole na shughuli zetu za usafi ziliendelea.
====>>Itaendelea wiki ijayo...
Endelea nayo: Tulifanya shughuli zetu kwa umakini mkubwa pasina hata kufuatiliwa na viongozi wetu jambo ambalo lilikuwa ni furaha kwetu. Mnamo saa 2 kamili asubuhi kengele ya kusanyiko la wanafunzi iligongwa na wanafunzi wote tulikusanyika mbele ya afisi kuu almaarufu kama “SMART AREA” ili kupewa maelekezo ya siku. Alisimama kiranja wa michezo na sanaa na kuanza kusema kwa sauti ya mashobo ya ujana , “Ndugu wanafunzi wenzangu, ninasimama mbele yenu nikiwa ni mwakilishi wenu wa masuala ya michezo hapa shuleni. Ni Imani yangu kwa ndani ya siku mbili zilizopita kumekuwa na tetesi ya kufanyika kwa sherehe ya kuwakaribisha wadogo zetu wa kidato cha kwanza mwaka huu. Kama ilivyo ada, kila mwaka sherehe hizi huambatana na uwepo wa wageni kutoka shule tofauti zenye mfumo wa kupokea watoto wa kike. Kwa kuwa shule yetu ndiyo kwanza imeanza kupokea wanafunzi wa jinsia ya kike, uongozi wa shule umeonelea vema uendelee na mtindo ule ule wa zamani kwa kuwaalika ndugu zetu wa shule za jirani. Kwa mwaka huu, wageni wetu watakuwa ni wanafunzi wa shule ya sekondari Kibondo. Sasa kazi ni kwenu katika kufanya maandalizi ya michezo mbalimbali kwani sherehe inatarajiwa kufanyika wiki ya mwisho ya mwezi huu wa April. Nadhani nimeeleweka kwa uzuri na ninaomba vijana wa vidato vya juu muwe walimu wa wadogo zetu ambao bado wamegubikwa na ushamba wa kutochangamkia fursa kama hizi ambazo hujitokeza mara moja au mbili kwa mwaka.”
Nilianza kufua nguo zangu kwa mpangilio maalum nikianzia na zile nilizochafua kwenye ile njozi niliyokusimulia awali, ambayo mpaka muda huu hakuna mtu yeyote nimekwisha msimulia zaidi yako wewe msomaji mpendwa ambaye najua hutanitangaza. Kwa kuwa sikuwa na nguo nyingi za kufua, nilifua taaratibu na kwa mbwembwe bila ktumia nguvu ya ziada ili kuepuka kuchanika kwa baadhi ya nguo zilizokuwa zimechakaa kwa kuchoshwa na uvaaji wa mara kwa mara. Nikiwa katikati ya safari yangu ya ufuaji, niligutushwa na vivuli vitatu vya watu vilivyojitokeza kwenye maji tulivu ya Ziwa Tanganyika ambayo hayakuwa na mawimbi makali siku hiyo. Mshtuko nilioupata haukuwa na mfano kwani mawazo yalinituma kwenye simulizi nilizowahi kuhadithia za wanyama hatari waishio baharini, mitoni au ziwani wenye sifa za kuwavutia binadamu majini kisha kuwanyonya damu na kuwasababishia umauti. Wanyama hawa walijulikana kwa jina la Chunusi. Kumbe haikuwa hivyo kwani nilipotaka kuchanganya mbarika zangu ili niisalimishe roho yangu, nilikutana MUJARABU na rafiki yangu Mood akiwa ameambatana na mabinti wawili ambaye mmoja nilimfahamu kwa jina la Fety, mwanafunzi mwenzetu wa kutwa ambaye hakuishi mbali na shule. Fety au Fatuma Mohamed alikuwa akiishi kwenye nyumba za serikali zilizopo mkabala na gereza la Bangwe.
Mapigo ya moyo wangu yalianza kurejea katika hali yake ya kawaida huku Mood akiendelea kunicheka sana kana kwamba uso wangu umekuwa kichekesho. Alicheka sana mpaka ushuzi ukamtoka pasina kujijua tena mbele ya watoto warembo kama hao aliokuja nao. Mpaka ninapokuhadithia simulizi hii sijawahi kumshuhudia tena mwanaume aliyejamba Mubashara mbele ya Maghashi bila hata kujali kama alivyofanya jamaa yangu. Niliacha zoezi la kufua kisha nikaanza kupokea utambulisho wa ugeni wa mabinti hao walioambatana na Mood kwa kutajiwa majina yao au wasifu wao kwa ujumla.
********
Baada ya matangazo hayo tulitawanyika kuelekea kupata vifungua kinywa kwa uji wa maziwa ambao shule ilizawadiwa vifuko vya maziwa ya unga kutoka shirika moja la kuwahudumia wakimbizi lenye masikani yake mjini Kasulu. Kwa wale ambao hatukuwa na ‘pocket’ money, tulijinywea uji ulio uchi kwa mtindo wa kikombe juu ya kikombe maarufu kama kupiga CHANYA lengo likiwa nikulijaza tumbo ili utumbo usijikunje. Baada ya kifungua kinywa kila mwanafunzi alielekea kwenye utawala wake binafsi. Nilikusanya nguo zangu za shule na zile za kushindia kisha nikazichanganya na matandiko, tayari kwa safari ya kwenda ziwani kufua. Kiukweli siku hiyo sikuwa na nguo chafu bali kilichonipeleka ziwani ni ile janaba la njozi pevu lililosababisha kuchafuka kwa matandiko yangu kana kwamba mchoma chips alikuja kunimwagia mabaki ya ute wa mayai. Niliungana na wenzangu pale ziwani katika ufuaji huku nikiwa nimejitenga pembeni kuficha aibu hiyo inayowatokea vijana barubaru waliofikia kipindi cha kubalehe. Zoezi la ufuaji liliendelea taratibu huku kichwani nikiwa na mawazo ya kuhudhuria au kutohudhuria sherehe hiyo ya kutukaribisha vijana wa kidato cha kwanza. Ingawa Jumamosi ni siku ya kufanya usafi kwa ujumla, siyo wote walioelekea ziwani kwa minajili ya kufua bali kuna waliofika beach kula BATA na wapendwa wao na wengine walijirusha kwa wandugu mitaani kwa lengo la kwenda kumendea misosi mbadala baada ya kuchoshwa na “fulu suti” yaani ugali kwa maharage wa kila siku. Kuna waliokwenda maeneo ya Mwanga sokoni kwa minajili ya kupata vinguo vya bei za mafungu kwenye soko la “SAGULA SAGULA” ili wajipatie suruali mdomo wa chupa ambazo siku hizi wamezibatiza jina la “MODO”. Mtindo wa uvaaji huu wa modo uliibuliwa na vijana toka mikoa ya Bandari Salama ulioambatana na suruali kuvaliwa nusu mlingoti ama kata “K”. Miongoni mwa wanafunzi ambao hatukuwa na ushabiki wa mavazi ni mimi na mood.
********
Nilianza kufua nguo zangu kwa mpangilio maalum nikianzia na zile nilizochafua kwenye ile njozi niliyokusimulia awali, ambayo mpaka muda huu hakuna mtu yeyote nimekwisha msimulia zaidi yako wewe msomaji mpendwa ambaye najua hutanitangaza. Kwa kuwa sikuwa na nguo nyingi za kufua, nilifua taaratibu na kwa mbwembwe bila ktumia nguvu ya ziada ili kuepuka kuchanika kwa baadhi ya nguo zilizokuwa zimechakaa kwa kuchoshwa na uvaaji wa mara kwa mara. Nikiwa katikati ya safari yangu ya ufuaji, niligutushwa na vivuli vitatu vya watu vilivyojitokeza kwenye maji tulivu ya Ziwa Tanganyika ambayo hayakuwa na mawimbi makali siku hiyo. Mshtuko nilioupata haukuwa na mfano kwani mawazo yalinituma kwenye simulizi nilizowahi kuhadithia za wanyama hatari waishio baharini, mitoni au ziwani wenye sifa za kuwavutia binadamu majini kisha kuwanyonya damu na kuwasababishia umauti. Wanyama hawa walijulikana kwa jina la Chunusi. Kumbe haikuwa hivyo kwani nilipotaka kuchanganya mbarika zangu ili niisalimishe roho yangu, nilikutana MUJARABU na rafiki yangu Mood akiwa ameambatana na mabinti wawili ambaye mmoja nilimfahamu kwa jina la Fety, mwanafunzi mwenzetu wa kutwa ambaye hakuishi mbali na shule. Fety au Fatuma Mohamed alikuwa akiishi kwenye nyumba za serikali zilizopo mkabala na gereza la Bangwe.
********
====>>Itaendelea wiki ijayo...
Usiikose SEHEMU YA 06>>> ya Riwaya hii ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo, na utaipata hapa Zero Degree pekee.
Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 05
Reviewed by Zero Degree
on
6/16/2017 12:14:00 PM
Rating: