Loading...

Hatimaye Ally Mayai Tembele amechukua fomu ya kuwania Urais wa TFF.


Ally Mayai Tembele amechukua fomu ya kuwania Urais wa Shirikisho la soka Tanzania bara [TFF].

Mayai sasa atachuana na Jamal Malinzi ambaye anashikilia nafasi hiyo. Lakini wako wengine kama; Athumani Nyamlani, Omar Madega na Wallace Karia ambao atalazimika kufanya kazi ya ziada kuwazidi.

Mayai ambaye amewahi kuwa nahodha wa Yanga alisindikizwa na wachezaji mbalimbali wa zamani wakiongozwa na Athumani Tippo, Jamhuri Kihwelo 'Julio'.


Wakati huo huo, Mtemi Ramadhani naye amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mtemi amechukua fomu hiyo leo akisindikizwa katika ofisi za TFF Karume jijini Dar es Salaam na baadhi ya wachezaji wa zamani.


Atakaochuana nao Mtemi ni Geofrey Nyange 'Kaburu', Michael Wambura na Mulamu Ng'ambi.

Mtemi alikuwa mshambuliaji hatari wa Simba pia Taifa Stars wakati huo akikipiga.

Hatimaye Ally Mayai Tembele amechukua fomu ya kuwania Urais wa TFF. Hatimaye Ally Mayai Tembele amechukua fomu ya kuwania Urais wa TFF. Reviewed by Zero Degree on 6/19/2017 03:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.