Loading...

Hatimaye Donald Ngoma amesaini mkataba mpya Yanga SC

Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aksaini mkataba wa miaka miwili leo mjini Dar es Salaam kuendelea kuichezea Yanga
Mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Ngoma aliwasili jana usiku Dar es Salaam baada ya taarifa kwamba amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na Polokwane City ya Afrika Kusini.

Lakini tangu jana mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga kabla ya leo mchana kusaini, hivyo pia kuzima tetesi za kwamba anataka kujiunga na mahasimu, Simba.

Ngoma ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga na wapinzani wa Yanga, Simba SC kabla ya kuzuka kwa taarifa za kujiunga na klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi ya kuu ya Afrika Kusini ‘Primiership ABS‘ ambapo alitua nchini usiku wa jana na mchana wa leo amesaini mkataba huo.
Hatimaye Donald Ngoma amesaini mkataba mpya Yanga SC Hatimaye Donald Ngoma amesaini mkataba mpya Yanga SC Reviewed by Zero Degree on 6/28/2017 04:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.