Liverpool, Chelsea zaingia vitani kusaka saini ya nyota huyu wa FC Porto
Nyota huyo mwenye miaka 20 ameanzia kikosi cha kwanza katika michezo mitatu ya timu yake ya taifa Ureno chini ya miaka 21 kwenye michuano iliyofanyika Poland.
Kwa mujibu wa 'A Bola' kiungo huyo yuko njiani kufuata pesa nono mbali na hapo FC Porto katika majira haya.
Liverpool na Chelsea zinaripotiwa kuwa miongoni mwa klabu kubwa za kwanza zinazoongoza katika vita ya kusaka saini ya Neves.
Hata hivyo, Inaripotiwa kuwa timu hizo mbili za Ligi Kuu ya Uingereza zinaweza kukumbana na ushindani mkubwa kutoka kwa Wababe wa Sirie A ya Italia, Juventus.
Porto tayari wamemuuza Andre Silva kwenda AC Milan kwa malipo ya awali ya uhamisho kiasi cha euro milioni 33 katika majira haya ya joto.

Na mtandao wa 'A Bola' unasema kwamba wareno hao (FC Porto) wako kwenye mawindo ya kiasi kama hicho hicho cha fedha kwa Ruben Neves.
Amekuwepo pale "Estadio do Dragao" tangu akiwa na umri wa miaka 8.
Lakini kinda huyo amekuwa na wakati mgumu sana kupata nafasi ya mara kwa mara kikosini kwa msimu huu, akipata kutokea uwanjani mara 18 tu katika mashindano yote.
Amesalia na miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa.
Amekuwepo pale "Estadio do Dragao" tangu akiwa na umri wa miaka 8.
Lakini kinda huyo amekuwa na wakati mgumu sana kupata nafasi ya mara kwa mara kikosini kwa msimu huu, akipata kutokea uwanjani mara 18 tu katika mashindano yote.
Amesalia na miaka miwili kwenye mkataba wake wa sasa.
Liverpool, Chelsea zaingia vitani kusaka saini ya nyota huyu wa FC Porto
Reviewed by Zero Degree
on
6/28/2017 12:47:00 PM
Rating: