Loading...

Hatimaye Hazard ametoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na 'future' yake Chelsea


Eden Hazard amefunga mjadala uliokuwa ukiendelea mitandaoni kuhusu suala la kutaka kutimukia Real Madrid katika majira haya ya joto.

Nyota huyo toka Ubelgiji amefuta tetesi zote kwa kusisitiza kwamba, bado anahitaji kubeba mataji mengi akiwa na Chelsea.

Hazard amekuwa akihusishwa na uhamisho kuelekea Bernabeu katika majira haya ya joto, hata hivyo, ripoti kutoka ndani ya Chelsea zinasema mchezaji huyo ameamua kujifunga na klabu yake kwa lengo la kuendelea kusaka mataji zaidi Stamford Bridge.

Hazard pia amedai kwamba ana sahuku kubwa ya kucheza pamoja na wachezaji wapya ambao wanategemewa kutua Chelsea.


“Naimani msimu ujao hautakuwa tofauti sana na huu ulioisha, na nina mategemeo makubwa ya kutwaa tena taji la ligi kuu na kisha kuwa mchezaji bora wa mwaka,” Hazard aliliambia gazeti la Chelsea.

“Kiukweli kushinda taji la Ligi ndicho tunahitaji kwa sana na kupewa tuzo ni kama 'bonus'.

“Tulianza msimu vizuri na kufanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu, lakini msimu ujao inatupasa kufanya kazi kubwa zaidi ya tuliyoifanya msimu huu. Tunatakiwa kuwa tayari kila mwaka katika ari ile ile ili kuwa juu ya wengine.

“Nimekuwepo hapa kwa miaka mitano sasa na nina furaha, baada ya miaka mitano hiyo ninaelewa mambo yote muhimu yanayoihusu klabu yangu. Pamoja na kwamba bado nina miaka 26, tayari nina uzoefu mkubwa sasa.

“Nilianza kucheza mpira nikiwa na umri wa miaka 16 Ufaransa, hivyo nimekuwa mchezaji wa kulipwa wa kimataifa kwa miaka 10. Katika suala la idadi ya mechi na uzoefu, mimi pia ni mmoja wa wakongwe.

“Naipenda Klabu hii kwa sababu ni kama sehemu ya familia kwangu. Ninao marafiki wengi na wote tuna mawasiliano mazuri na ukijaribu kuangalia nimekuwa katika kiwango cha juu karibuni kwa kila mchezo katika msimu uliopita hivyo nilikuwa na furaha na kiwango nilichokuwa nacho.

“Ninajua kwamba, kama nitafunga ninaweza kuisaidi timu yangu kupata ushindi, na katika mfumo mpya nimekuwa karibu sana na goli hivyo imekuwa rahisi kupenya, kutoa 'assist' na kufunga magoli ya kutosha.” alisema Hazard.
Hatimaye Hazard ametoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na 'future' yake Chelsea Hatimaye Hazard ametoa uamuzi wa mwisho kuhusiana na 'future' yake Chelsea Reviewed by Zero Degree on 6/17/2017 10:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.