Loading...

Kesi ya Pedeshee Ndama 'Mtoto wa Ng'ombe' yapigwa kalenda


Kesi inayomkabili mfanyabiashara, Shabani Hussein maarufu Pedeshee Ndama Mtoto wa Ng'ombe imeahirishwa hadi Julai 20, 2017 baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi bado haujakamilika.

Ndama ambaye kwa sasa yupo nje kwa dhamana, kesi yake ilitajwa jana (Ijumaa) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Ndama kwa sasa anakabiliwa na mashtaka matano baada ya kulikubali shtaka la sita la kutakatisha fedha na kisha kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini ya shilingi milioni 200.

Hatua yake ya kulipa kiasi hicho cha fedha, ilimuepusha na kifungo cha miaka mitano jela.

Ndama yupo huru pia kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambapo kila mdhamini alisaini bondi ya shilingi milioni 100.

Pia mshtakiwa mwenyewe aliweka hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Dola 270,200 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 600.
Kesi ya Pedeshee Ndama 'Mtoto wa Ng'ombe' yapigwa kalenda Kesi ya Pedeshee Ndama 'Mtoto wa Ng'ombe' yapigwa kalenda Reviewed by Zero Degree on 6/17/2017 10:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.