Loading...

Hivi ndivyo ilivyo kuhusiana na suala zima la usajili wa Niyonzima hadi hivi sasa


Taarifa za usajili wa kiungo Haruna Niyonzima, zimeendelea kuzua mjadala mkubwa mitandaoni.

Kuna taarifa zinadai kwamba tayari Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili Simba na wengine wanadai ameongeza mkataba Yanga.

Habari kutoka kwa rafiki wa Niyonzima, zimeeleza hadi sasa kiungo huyo Mnyarwanda hajasaini upande wowote ule.

“Niyonzima hajasaini Simba wala Yanga, haya ni maneno tu ya watu ndugu yangu. Lakini tutajua baadaye au siku nyingine,” kilieleza chanzo.

Niyonzima amekuwa akiwaniwa na Simba baada ya kuichezea Yanga kwa misimu sita akitokea APR ya Rwanda.
Hivi ndivyo ilivyo kuhusiana na suala zima la usajili wa Niyonzima hadi hivi sasa Hivi ndivyo ilivyo kuhusiana na suala zima la usajili wa Niyonzima hadi hivi sasa Reviewed by Zero Degree on 6/18/2017 11:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.