Loading...

Waziri Mwigulu afunguka kuhusu Mkapa na Kikwete kuhusishwa na sakata la Makinikia


Ikiwa zimepita siku chache tangu Rais Magufuli kuzuia watu kuwahusisha Marais wawili wastaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa katika sakata la mchanga wa dhahabu (makinikia) kwani katika ripoti zote mbili hakuna sehemu ambayo imewataja wastaafu kuhusika.

Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema wezi hao walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostaafu ili kuzia serikali iache kufatilia sakata hilo.

“Viongozi wetu hawajawai kuwa mawakala wa wale wanaotuibia, mawakala tumewabaini ni wale wanao watetea wezi,” 

”Kwa imani zetu wote, tuendelee kumuombea Rais wa nchi yetu, Rais wetu mpendwa kwa kazi kubwa anazozifanya ambazo zitasaidi hii mipango mingi tunayopanga kwenye majimbo yetu, matamanio na matarajio yetu mengi tunayokuwa nayo katika majimbo yetu.

“Ukizunguka kote jibu lake linakuja mahitaji ya fedha. Barabara mahitaji ya fedha; elimu bure mahitaji ya fedha, maji mahitaji ya fedha, umeme mahitaji ya fedha, Hospitali huduma bure mahitaji ya fedha. Hicho ndicho kinachomuuma Rais mpaka munaona anachukua hatua ngumu zinazohitaji ujasiri kama anavyofanya.

“Kwa Mtanzania yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu lazima ataunga mkono juhudi hizo lakini kwa ambaye ana mambo yake ya ubinafsi na ametanguliza ubinafsi anaweza asielewe kazi inayofanywa lakini sisi ambao tunahitaji maji; tunaohitaji barabara, tunaohitaji elimu bure, tunaohitaji Hospitalini dawa ziwepo, tunaohitaji umeme, sote kwa maombi na kwa jitihada na hata kwa kusema tumuunge mkono Rais wetu kwa uzalendo na ujasiri mkubwa aliouonesha.” – Mwigulu Nchemba.

Waziri Mwigulu ameongeza kusema sifa ambayo inafanya viongozi walioko madarakani wasing’ang’anie madaraka ni viongozi wastaafu kuheshimiwa baada ya muda wa uongozi.

Waziri Mwigulu ameyaongea hayo akiwa katika kijiji cha Zinzirigi katika Tarafa ya Ndago katika mwendelezo wa ziara ya jimboni kwake Iramba Magharibi kuongea na wananchi kuwaeleza alipofikia kuhusu ahadi ambazo walikubaliana kutekeleza hasa suala la umeme kutokufika katika vijiji vingi akieleza kuwa sababu ni mkandarasi aliyekuwepo mkoa wa Singida aliyetolewa baada ya kushindwa kazi lakini sasa ameambiwa na watu wa wizara ya nishati kuwa wakandarasi wawili wameshapatikana hivyo kuanzia sasa zoezi la kuunganisha umeme vijijini litaendelea kwa kasi hasa wa REA awamu ya Tatu.

Kuhusu ujenzi wa zahanati amesema mpaka sasa zahanati katika vijiji vingi alipopita zimefika hatua nzuri ya kupaua na kuahidi kuwapelekea mabati na mbao na mifuko ya saruji 100 ili zahanati hizo zikamilike na kuanza kutoa huduma mapema sana.
Waziri Mwigulu afunguka kuhusu Mkapa na Kikwete kuhusishwa na sakata la Makinikia Waziri Mwigulu afunguka kuhusu Mkapa na Kikwete kuhusishwa na sakata la Makinikia Reviewed by Zero Degree on 6/18/2017 11:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.