Loading...

John Bocco amekabidhiwa jezi rasmi, yuko tayari kuianza kazi yake Simba SC


Baada ya viongozi wa Simba jana kumtambulisha Shomari Kapombe leo Juni 13, 2017 klabu ya Simba imemtambulisha rasmi nahodha wa zamani wa Azam FC John Bocco ‘Adebayor’.

Mshambuliaji mpya wa Simba, John Raphael Bocco, yuko tayari kuanza kazi yake na kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.

Bocco amejiunga na Simba akitokea Azam FC ambayo imeamua kubana matumizi.

Straika huyo mkongwe amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba ina nafasi ya kuutumia uzoefu wa Bocco wa zaidi ya misimu saba kwenye Ligi Kuu Bara.

Naye anaonekana yuko tayari na kazi baada ya kukabidhiwa jezi yake rasmi.

Aishi Manula ni mchezaji mwingine wa Azam ambaye tayari amesha mwaga wino kuitumikia Simba kwa mkataba wa miaka miwili lakini yeye bado hajatambulishwa rasmi kuwa ni mchezaji wa Simba.
John Bocco amekabidhiwa jezi rasmi, yuko tayari kuianza kazi yake Simba SC John Bocco amekabidhiwa jezi rasmi, yuko tayari kuianza kazi yake Simba SC Reviewed by Zero Degree on 6/13/2017 07:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.