Loading...

Bakayoko kutua London wiki ijayo kwa ajili ya Vipimo vya Afya

Kwa mujibu wa ripoti, ofa ya paundi milioni 35 tayari iko mezani kwa ajili ya Timoue Bakayoko na utaratibu wa vipimo vya Afya uko umeshaandaliwa.

'The Times' wanaripoti kwamba , maelewano tayari yamekwishafikiwa kwenye dili hilo la kumnasa Bakayoko na tayari atakuwa anaelekea Stamford Bridge kwa paundi milioni 35.

Inaripotiwa kwamba nyota huyo yuko tayari kukubaliana na utaratibu aliopewa na yuko kwenye harakati za kuelekea London kwa ajili ya vipimo vya afya wiki ijayo.

'The Times' pia wanasema kwamba, Michy Batshuayi anaweza kuelekea huko huko akitumika kama sehemu ya ofa ya kumnasa mchezaji mwingine toka hapo (Monaco).

Straika huyo wa Ubelgiji amekuwa akiripotiwa na mitandao mbalimbali akihusishwa na suala la kuelekea Monaco kwa mkopo au moja kwa moja na anaipa nafasi kubwa Ufaransa ukiachilia ofa ya kwenda Everton.
Bakayoko kutua London wiki ijayo kwa ajili ya Vipimo vya Afya Bakayoko kutua London wiki ijayo kwa ajili ya Vipimo vya Afya Reviewed by Zero Degree on 6/13/2017 07:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.