Loading...

Michy Batshuayi kutumika kumnasa Kylian Mbappe

Kwa mujibu wa ripoti, Antonio Conte yuko tayari kufanya mazungumzo pamoja na kylian Mbappe na michy Batshuayi anaweza kuwa sehemu ya makubaliano katika kumnasa nyota huyo.


Ripoti zinasema kwamba, Chelsea wanajipanga kupeleka ofa Monaco, tetesi hizi zimeanzia nchini Ufaransa.

'Le10 Sport' wanadai kwamba, 'The Blues' wamekwishafanya mawasiliano na kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 na Antonio Conte atakaa mezani kwa mazungumzo zaidi na nyota huyo baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Ufaransa na Uingereza tarehe 13 Juni.

Real Madrid na wapinzani wa Chelsea kwenye Ligi kuu ya Uingereza, Arsenal pia walihusishwa na kutaka kumsajili nyota huyo na ripoti toka Spain zinadai kwamba Zinedine Zidane yuko tayari yuko tayari kuiondoa Arsenal kwenye mbio hizo kwa kuweka ofa ya paundi milioni 100.

Michy Batshuayi
Hata hivyo, Chelsea wanampango wa kupeleka ofa kubwa tofauti na wengine na wako tayari kucheza na hisia walizonazo Monaco kwa Michy Batshuayi.

Mabingwa hao wa Ligi kuu ya Uingereza (2016/17) wako tayari kumtumia nyota huyo wa Ubeligiji ambaye kwa kiasi fulani ameshindwa kuonyesha makali tangu kuwasili kwake Chelsea kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 33 kutokea Marseille katika majira ya joto mwaka jana, kutumika kama sehemu ya dili la kumnasa Mbappe.

Inasemekana Monaco wanamuhitaji Batshuayi kwa hali na mali.
Michy Batshuayi kutumika kumnasa Kylian Mbappe Michy Batshuayi kutumika kumnasa Kylian Mbappe Reviewed by Zero Degree on 6/09/2017 03:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.