Loading...

Q Chief amtabiria mambo makubwa Chid Benz, ..adai hali aliyopitia hata yeye aliwahi kupitia


Msanii Q Chief amefunguka kwa kudai ameamua kumrudisha tena mkali wa 'free style' Chid Benz katika ulimwengu wa muziki.

Q Chief amebainisha hayo baada ya kusambaa picha mtandaoni zilizokuwa zinawaonyesha wawili hao wakiwa studio ambapo watu wengi walianza kujiuliza maswali yasiyokuwa na majibu ndani yake.



"Chid Benz ni moja kati ya ma-rapa ambao wanahistoria kubwa sana katika ukanda huu wa East Afrika, pia unapomzungumzia Chid Benz unamzungumzia moja kati ya rapa ambao wana tuzo zaidi ya tatu au nne za Hip hop na 'so far' nikijaribu kuangalia kwa Tanzania nani amechukua tuzo tatu, nne nawaona Weusi" alisema Q Chief.

Pamoja na hayo, Q chief amesema maisha aliyopitia swahiba wake Chid Benz hata yeye ameyapitia hivyo hajisikii vizuri kuona anamuacha bila ya kumsaidia kwa namna moja ama nyingine.

"Rashid ni rapa mzuri amepitia kwenye 'situation' ambazo hata mimi niliwahi kupitia. Nilishawahi kuhojiwa na mtandao mmoja mkubwa Tanzania nikaulizwa unadhani nini kifanyike kwa Rashidi, kikubwa nilichokisema ndicho kilichofanyika, nilisema kwamba dawa ya Rashid anayo yeye mwenyewe hatuna sisi, yeye mwenyewe ana tiba yake na tiba ni kukubaliana na nafsi yako kwamba upo kwenye giza unahitaji kwenda kwenye nuru. Nilichokifanya mimi ni kumsogeza Rashidi karibu na Mwenyezi Mungu kwa sababu tunaishi lazima tujue kuna Mungu" aliongezea Q chief.
Q Chief amtabiria mambo makubwa Chid Benz, ..adai hali aliyopitia hata yeye aliwahi kupitia Q Chief amtabiria mambo makubwa Chid Benz, ..adai hali aliyopitia hata yeye aliwahi kupitia Reviewed by Zero Degree on 6/09/2017 02:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.