Loading...

Mabaki ya ndege ya Myanmar na maiti za abiria zapatikana baharini

Picha ya maktaba ya ndege ya jeshi la angani la Myanmar muundo wa Y-8
Jeshi la Burma limesema kuwa mabaki ya ndege yake iliyotoweka Jumatano katika anga ya bahari ya Andaman ikiwa imebeba abiria 122 wengi wao wanajeshi na familia zao, yamepatikana.

Mabaki ya ndege na maiti zimepatikana katika bahari ya Andaman, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya jeshi.

Ndege hiyo aina ya Y8, iliyotengezwa nchini China, ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto.


Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Myeik ikielekea Yangon.

Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa tu, wakati ilipopoteza mawasiliano siku ya Jumatano.

Ndege hiyo ilinunuliwa kutoka China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa 809.

Myanmar imekumbwa na ajali kadhaa za ndege miaka ya hivi karibuni. Lakini ajali hii ya sasa ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi, walifariki baada ya ndege yao kuanguka kwenye mji mkuu wa Nay Pyi Taw.

Miezi mitatu baadaye maafisa watatu, waliuwawa wakati helikopta ya jeshi ilipoanguka katikati mwa Myanmar.

Source: BBC Swahili
Mabaki ya ndege ya Myanmar na maiti za abiria zapatikana baharini Mabaki ya ndege ya Myanmar na maiti za abiria zapatikana baharini Reviewed by Zero Degree on 6/08/2017 11:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.