Loading...

Mashabiki 1000 wa soka wamejeruhiwa kwenye mkanyagano uliotokea baada ya fataki kuzua hofu nchini Italia

Mashabiki wa kandanda takribani 1000 wajeruhiwa kwenye mkanyagano uliotokea nchini Italia
Takriban watu 1000 wamejeruhiwa katika mji wa Turin nchini Italia baada ya fataki kuzua hofu na kusababisha mkanyagano usiku wa Jumamosi kwa mujibu wa polisi.



Maelfu ya mashabiki wa kandanda walikuwa wakitazama mechi iliyokuwa ikipeperushwa moja kwa moja ya fainali ya kombe la UEFA kati ya Juventus na Real Madrid, wakati uvumi wa mlipuko ulianza kusambaa.

Takriban watu wawili akiwemo mtoto wa umri wa miaka 7 walijeruhiwa vibaya.

Real Madrid iliishinda Juventus kwa mabao 4-1 na kushinda kombe kwa mara ya 12.

Dakia kumi kabla ya kukamilika mwa mechi umati ulikimbia kutoka katikati ya eneo la Piazza San Carlo, na kuwasukuma watu kuelekea kwa vizuizi vilivyokuwa kando kando mwa eneo hilo.

Mikoba na viatu viliachwa vimetabakaa wakati watu walikimbia wakipiga nduru kutoka eno hilo.

Kwa mashabikia wa Jeventus kisa hicho kilifufua kumbukumbu za mwaka 1985 katika uwanja wa Heysel wakati watu 39 wengine wao mashabiki wa Italia, waliuawa wakati ukuta uliwaporomokea kabla ya fainali na Liverpool.
Mashabiki 1000 wa soka wamejeruhiwa kwenye mkanyagano uliotokea baada ya fataki kuzua hofu nchini Italia Mashabiki 1000 wa soka wamejeruhiwa kwenye mkanyagano uliotokea baada ya fataki kuzua hofu nchini Italia Reviewed by Zero Degree on 6/04/2017 01:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.