Loading...

Watu 7 wameuwawa katika shambulio jingine la kigaidi nchini Uingereza

Watu sita wameuawa na wengine 48 kujeruhiwa katika shambulio linalodaiwa kuwa la kigaidi leo, jijini London, Uingereza.

Polisi nchini humo wamesema, polisi walifanikiwa kuwaua washambuliaji watatu kati yao.

Ghasia zilianza baada ya gari moja kuingia ndani ya umati wa watembea miguu, katika daraja kuu jijini London.

Taarifa zimesema watu 20 waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali sita tofauti jijini London.

Mwandishi wa BBC Holly Jones, aliyekuwepo katika eneo hilo wakati wa shambulio hilo amesema gari lililohusika lilikuwa linaendeshwa na mwanamume na lilikuwa linaenda kwa kasi.


"Alilipinda gari karibu nami na akagonga watu watano au saba hivi. Aliwagonga wawili mbele yangu na kisha wengine watatu waliokuwa nyuma yangu," Jones ameiambia BBC. 



Watu 7 wameuwawa katika shambulio jingine la kigaidi nchini Uingereza Watu 7 wameuwawa katika shambulio jingine la kigaidi nchini Uingereza Reviewed by Zero Degree on 6/04/2017 12:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.