Loading...

Mfalme wa Morocco asusia mkutano wa Ecowas

Mfalme wa Morocco, Mohammed VI
Waziri mkuu wa Israel , Benjamin Netanyahu, ameuambia mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika magharibi kwamba uhusiano madhubuti na nchi barani Africa ilikuwa ni fursa tosha kwa nchi yake , Israel.

Hata hivyo Mfalme wa Morocco, Mohammed wa sita , alighairi kushiriki katika mkutano huo kwa sababu bwana Netanyahu alithibitisha ushiriki wake.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida vyombo vya habari nchini Israel viliripoti kwamba timu ya walinzi wa bwana Netanyahu walihusika katika prukushani kiasi cha kushikana mwilini huku wakisukumana na waliniz wa rais wa Tofo Faure Gnassingbe.

Wakati wa mkutano huo, raisi Gnassingbe alichaguliwa kushika nafasi ya kuwa mwenyekiti wa bodi ya Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) akichukua nafasi ya rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf.
Mfalme wa Morocco asusia mkutano wa Ecowas Mfalme wa Morocco asusia mkutano wa Ecowas Reviewed by Zero Degree on 6/05/2017 09:09:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.