Loading...

Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake wamekamatwa na TAKUKURU


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kupelekwa Polisi kwa ajili ya uchunguzi dhidi yao kwa tuhuma za rushwa.

Hilo limethibitisha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba ambaye amesema taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao, kwa sasa ifahamike kuwa viongozi hao wanawashikilia.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walipelekwa Sentro jana na leo asubuhi wamepelekwa Makao Makuu ya Takukuru kwa ajili ya uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake wamekamatwa na TAKUKURU Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake wamekamatwa na TAKUKURU Reviewed by Zero Degree on 6/28/2017 12:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.