Loading...

Rais wa Visiwa vya Vanuatu afariki dunia ghafla kwa mshtuko wa moyo

 Rais wa visiwa vya Vanuatu, Baldwin Lonsdale wakati wa uhai wake 
Rais wa visiwa vya Vanuatu, Baldwin Lonsdale amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mshtuko wa moyo jana.

Lonsdale ambaye pia ni Kasisi wa Anglikana amekuwa kiongozi wa kisiwa hicho cha Pacific kwa miaka miwili tangu Septemba 2014.

Gazeti la Daily Post nchini Vanuatu limesema kuwa Lonsdale alifariki ghafla kwenye mji mkuu wa Port Vila usiku wa kuamkia jana.

Akiwa rais, Lonsdale aliongoza ujenzi mpya wa maeneo ya kisiwa hicho kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga cha Pam kilichosababisha watu 75,000 kukosa makazi mwezi Machi mwaka 2015.

Oktoba mwaka huohuo aliapa kupambana na ufisadi nchini humo baada ya sakata lililomhusisha makamu wake la matumizi mabaya ya rasilimali za umma.
Rais wa Visiwa vya Vanuatu afariki dunia ghafla kwa mshtuko wa moyo Rais wa Visiwa vya Vanuatu afariki dunia ghafla kwa mshtuko wa moyo Reviewed by Zero Degree on 6/18/2017 09:34:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.