Serikali imesaini mkataba wa kuboresha Bandari ya Dar es Salaam
Akizungumza na wadaua mbalimbali wa bandari Waziri wa Uchukuzi na Mawasilino Profesa Makame Mbarawa amesema kwa sasa Bandari ya Dar es Salaam haiweze kupokea meli kubwa ambazo ndizo zinatumika kwa sasa na makampuni ya kimataifa na ndio maana wameona ni vyema waiboreshe bandari.
Naye Mkurugenzi mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema ujenzi huo utagharimu dola za kimarekani Milioni 336 na ujenzi utafanyika kwa kipindi cha miezi 36 huku kampuni inayojenga bandari hiyo ya China Habour Einfering ikisema imejipanga vyema kufanya kazi hiyo.
Baadhi ya wadau waliofika katika hafla hiyo wamesema wana matumaini makubwa na bandari hiyo na hasa katika mpango wake wa sasa wa kuiboresha kwani itasaidia kuongeza idadi ya mizigo inayopita Dar es Salaam na wakiwa kama wadau watafanya kazi vizuri zaidi.
Serikali imesaini mkataba wa kuboresha Bandari ya Dar es Salaam
Reviewed by Zero Degree
on
6/11/2017 01:33:00 PM
Rating: