Loading...

Shabiki mkubwa wa Yanga maarufu kwa jina la Ally Yanga afariki Dunia

Marehemu Ally Yanga enzi za uhai wake
Uongozi wa klabu ya Yanga SC umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyekuwa shabiki wao mkubwa aliyefahamika kwa jina la Ally Yanga.


Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema kifo cha shabiki huyo kimeacha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa pamoja na kuwa balozi mzuri kama mwananchama wa timu hiyo.

Enzi za uhai wake Ally Yanga atakumbukwa kutokana na mbwembwe zake alizokuwa akizionesha za kujipaka masizi ya mkaa usoni pindi klabu ya Yanga ikiwa uwanjani.

Taarifa zinaeleza, Ally Yanga amefariki dunia katika ajali ya gari huko Mpwapwa mkoani Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amethibitisha kwamba ajali hiyo imetokea leo mchana na Ally amepoteza maisha.
Shabiki mkubwa wa Yanga maarufu kwa jina la Ally Yanga afariki Dunia Shabiki mkubwa wa Yanga maarufu kwa jina la Ally Yanga afariki Dunia Reviewed by Zero Degree on 6/20/2017 11:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.