Sigara inavyoedelea kuwa tishio Bongo
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu |
Hayo yamo kwenye taarifa ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, iliyosomwa kwa niaba yake na Mratibu Magonjwa yasiyoambukiza, Dk. Sarah Maongezi, kutoka wizarani hapo wakati wa maadhimisho ya siku ya kutotumia tumbaku duniani.
Maadhimisho hayo ambayo yaliandaliwa na Chama cha Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku Tanzania (TTCF) kwa mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu isemayo ‘Tumbaku tishio kwa maendeleo’.
Ummy alisema uchunguzi uliofanywa mwaka 2013 na wizara hiyo, taasisi ya Utafiti wa Maradhi ya Binadamu wakishirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), ulionyesha wastani wa asilimia 14 ya Watanzania wanatumia tumbaku.
Pia alisema asilimia 17.5 wanavutishwa moshi majumbani na asilimia 24.9 wanavutishwa sehemu za kazi.
Waziri Ummy alisema wizara yake itahakikisha inasimamia uundwaji wa sheria na utekelezaji wake ili kukabiliana na tatizo hilo.
Pia alisema watahakikisha kuanzia sasa paketi zote za sigara zinazotengenezwa au kuingizwa nchini zinakuwa na maandishi ya onyo la madhara ya tumbaku yanayosomeka mbele na nyuma ya paketi.
Pia alisema ipo kamati maalum iliyoundwa kwa kushirikiana na wizara nyingine pamoja na asasi za kiraia ili kuchambua na kushauri kitaalamu udhibiti wa bidhaa hiyo.
Mwalimu alisema kuongeza kodi kwenye bidhaa za tumbaku ni mkakati unaoweza kugharamia mpango wa afya kwa wote na programu nyingine serikalini.
Alisema takwimu za dunia zinaonyesha takribani watu milioni 6 kila mwaka hufariki kutokana na tumbaku na zaidi ya watu 600,000 hufa kutokana na kuvuta moshi wake kila mwaka.
Alisema hali hiyo isipodhibitiwa inakadiriwa ifikapo mwaka 2030, vifo hivyo vitaongezeka hadi watu milioni 8 kwa mwaka na asilimia 80 ya vifo hivyo vitatokea nchi zinazoendelea, ikiwamo Tanzania.
Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dk. Matshidiso Moeti, katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Dk. Neema Kileo, alisema karibu vijana 146,000 kwenye umri kuanzia miaka 30 hufa kila mwaka kwa magonjwa yatokanayo na tumbaku.
Mkurugenzi wa TTCF, Lutgard Kagaruki, alisema mapambano ya kupinga matumizi ya tumbaku ni magumu na kuomba vyuo kikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuwa cha mfano kwa kuweka mabango ya kupinga uvutaji sigara.
Pia alisema utungwaji wa sheria na kuitekeleza kama alivyoahidi Waziri Ummy utakifanya chama hicho kipumue kwa sababu itawezesha kudhibiti matumizi ya tumbaku. Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa UDSM, Dk. Mona Mwakalinga, ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Umma chuoni hapo, aliwataka wanafunzi kutoa elimu kwa wazazi na walezi kuhusu madhara ya tumbaku.
Maadhimisho hayo ambayo yaliandaliwa na Chama cha Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku Tanzania (TTCF) kwa mwaka huu yamebebwa na kaulimbiu isemayo ‘Tumbaku tishio kwa maendeleo’.
Ummy alisema uchunguzi uliofanywa mwaka 2013 na wizara hiyo, taasisi ya Utafiti wa Maradhi ya Binadamu wakishirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), ulionyesha wastani wa asilimia 14 ya Watanzania wanatumia tumbaku.
Pia alisema asilimia 17.5 wanavutishwa moshi majumbani na asilimia 24.9 wanavutishwa sehemu za kazi.
Waziri Ummy alisema wizara yake itahakikisha inasimamia uundwaji wa sheria na utekelezaji wake ili kukabiliana na tatizo hilo.
Pia alisema watahakikisha kuanzia sasa paketi zote za sigara zinazotengenezwa au kuingizwa nchini zinakuwa na maandishi ya onyo la madhara ya tumbaku yanayosomeka mbele na nyuma ya paketi.
“Tutahakikisha hakuna matangazo ya tumbaku kwenye mabango barabarani, runinga, redio, sinema au matangazo kupitia magari ya matangazo,” alisema.
Mwalimu alisema kuongeza kodi kwenye bidhaa za tumbaku ni mkakati unaoweza kugharamia mpango wa afya kwa wote na programu nyingine serikalini.
Alisema takwimu za dunia zinaonyesha takribani watu milioni 6 kila mwaka hufariki kutokana na tumbaku na zaidi ya watu 600,000 hufa kutokana na kuvuta moshi wake kila mwaka.
Alisema hali hiyo isipodhibitiwa inakadiriwa ifikapo mwaka 2030, vifo hivyo vitaongezeka hadi watu milioni 8 kwa mwaka na asilimia 80 ya vifo hivyo vitatokea nchi zinazoendelea, ikiwamo Tanzania.
Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dk. Matshidiso Moeti, katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Dk. Neema Kileo, alisema karibu vijana 146,000 kwenye umri kuanzia miaka 30 hufa kila mwaka kwa magonjwa yatokanayo na tumbaku.
“Takribani wastani wa watumiaji wote wanapoteza miaka 15 ya kuishi mbele, hii inafanya uvutaji wa sigara kuwa moja ya hatari zinazoweza kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kama moyo, saratani, magonjwa ya mapafu na sukari,” alisema.
Mkurugenzi wa TTCF, Lutgard Kagaruki, alisema mapambano ya kupinga matumizi ya tumbaku ni magumu na kuomba vyuo kikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuwa cha mfano kwa kuweka mabango ya kupinga uvutaji sigara.
Pia alisema utungwaji wa sheria na kuitekeleza kama alivyoahidi Waziri Ummy utakifanya chama hicho kipumue kwa sababu itawezesha kudhibiti matumizi ya tumbaku. Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa UDSM, Dk. Mona Mwakalinga, ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Umma chuoni hapo, aliwataka wanafunzi kutoa elimu kwa wazazi na walezi kuhusu madhara ya tumbaku.
Sigara inavyoedelea kuwa tishio Bongo
Reviewed by Zero Degree
on
6/01/2017 09:29:00 AM
Rating: