Tanzania imeshuka nafasi 4 katika viwango vipya vya Soka duniani
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetoa orodha ya viwango vya soka duniani kwa mwezi Mei, 2017 ambapo kwa Tanzania hali ni mbaya baada ya kushuka kwa nafasi nne.
Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 135 hadi nafasi ya 139, jambo ambalo kisoka sio zuri na kumaanisha kuwa bado tupo chini kwa uwezo wa kucheza mchezo huo pendwa duniani.
Nafasi ya kwanza kwenye viwango hivyo imeshikwa na Brazil wakifuatiwa na Argentina, Ujerumani, Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Switzerland na Hispani ikishika nafasi ya kumi.
Kwa upande wa Afrika, Misri inaongoza ikifuatiwa na Senegal, Cameroon, Nigeria, Congo DRC, Tunisia, Burkina Faso, Ivory Coast, Ghana, Algeria na Morocco ikiwa kwenye nafasi ya kumi.
Nafasi ya kwanza kwenye viwango hivyo imeshikwa na Brazil wakifuatiwa na Argentina, Ujerumani, Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Switzerland na Hispani ikishika nafasi ya kumi.
Kwa upande wa Afrika, Misri inaongoza ikifuatiwa na Senegal, Cameroon, Nigeria, Congo DRC, Tunisia, Burkina Faso, Ivory Coast, Ghana, Algeria na Morocco ikiwa kwenye nafasi ya kumi.
Tanzania imeshuka nafasi 4 katika viwango vipya vya Soka duniani
Reviewed by Zero Degree
on
6/01/2017 05:39:00 PM
Rating: