Loading...

Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanaotumia madaraka yao vibaya waonywa


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI Mhe.GEORGE SIMBACHAWENE amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia mamlaka yao vibaya ya kuwaweka ndani viongozi,watumishi wa umma na wananchi wengine kwa uonevu kwa kisingizio cha sheria kuwapa mamlaka hayo.

Kauli hiyo ya Waziri SIMBACHAWENE ameitoa bungeni ikiwa ni baada ya wabunge kuhoji uwepo wa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kutoa amri ya kukamatwa kwa watu bila sababu ya msingi hivyo ni hatua gani serikali inachukua dhidi yao kukomesha tabia hiyo.

Amesema licha ya sheria kuwapa viongozi hao mamlaka hayo wanapaswa kuwa makini wanapoitumia kama sheria inavyotamka kwa kuzingatia mipaka yao ya kazi katika kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa.

Sheria ya tawala za mikoa ya mwaka 1997 sura ya 97 inawapa mamlaka wakuu wa mikoa na wilaya kumweka ndani mtu ye yote kwa muda wa saa48 ikiwa itathibitika kuna hatari ya uvunjifu wa amani na usalama au mtu huyo ametenda kosa la jinai.
Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanaotumia madaraka yao vibaya waonywa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanaotumia madaraka yao vibaya waonywa Reviewed by Zero Degree on 6/16/2017 08:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.