Watu zaidi ya 15 hawajulikani walipo baada ya Jengo la ghorofa 7 kuanguka nchini Kenya
Zaidi ya watu 15 hawajulikani walipo baada ya jengo la ghorofa saba kuanguka usiku wa kuamkia leo, katika kijiji cha Kware, Embakasi, Nairobi.
The Daily Nation (mtandaoni) limeandika kuwa watu zaidi ya 120 wameokolewa baada ya kufunikwa na kifusi wakati jengo hilo lilipoanguka.
Akihojiwa na gazeti hilo, Joas Nemati, mmoja wa wapangaji katika jengo hilo amesema, mafundi walionekana jana saa 7 mchana wakikarabati ufa mkubwa uliokuwa katika jengo hilo katika moja ya ngazi na wakawahakikishia wapangaji hao kuwa lipo salama.
Mratibu wa shughuli za uokoaji Pius Masai amesema kuwa zaidi ya watu 100 wameokolewa lakini akaongeza kuwa huenda watu wengi zaidi wamekwama.
Aprili mwaka huu, watu 49 walifariki dunia nchini humo wakati jengo jingine la ghorofa lilipoporomoka baada ya mvua kubwa kunyesha.
Akihojiwa na gazeti hilo, Joas Nemati, mmoja wa wapangaji katika jengo hilo amesema, mafundi walionekana jana saa 7 mchana wakikarabati ufa mkubwa uliokuwa katika jengo hilo katika moja ya ngazi na wakawahakikishia wapangaji hao kuwa lipo salama.
“Lakini ilipofika saa 12 jioni mke wa Nemati alimuita na kumwambia kuwa wapangaji wameambiwa waondoke haraka kwa kuwa jengo hilo linaanguka,” amesema.
Aprili mwaka huu, watu 49 walifariki dunia nchini humo wakati jengo jingine la ghorofa lilipoporomoka baada ya mvua kubwa kunyesha.
Watu zaidi ya 15 hawajulikani walipo baada ya Jengo la ghorofa 7 kuanguka nchini Kenya
Reviewed by Zero Degree
on
6/13/2017 02:31:00 PM
Rating: