Zoezi la kuhakiki 'Bodaboda' jijini Dar linaendelea
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Hawa Mwaifunga (Chadema). Mwaifunga alitaka kujua serikali ina utaratibu gani wa kuhakiki na kutambua wamiliki, madeveva na mahali zinapoegesha bodoboda na bajaji. Mwigulu alisema, serikali inahakiki pikipiki na bajaji kwa kushirikiana na serikali za mitaa na halmashauri za jiji hilo.
Aidha, kupitia usajili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na serikali za mitaa, halmashauri ya jiji hilo zimeendelea kuhakiki vyombo hivyo vya usafiri pamoja na kuanzisha utaratibu wa kuvisajili. “Pikipiki na bajaji zinasajiliwa katika maeneo ya maegesho ili kupta kumbukumbu za mmiliki, dereva na eneo lake maalumu la kuegesha,” alisema.
Alisema serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kutokana na kuongezeka kwa uhalifu unaofanywa na waendesha bodaboda na bajaji jijini humo. Hivyo, “serikali kupitia jeshi la polisi imekuwa ikichukua hatua za kufanya doria kwa magari, pikipiki na kutembea kwa miguu na kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi shirikishi ili kubaini na kuzuia uhalifu”.
Zoezi la kuhakiki 'Bodaboda' jijini Dar linaendelea
Reviewed by Zero Degree
on
6/13/2017 03:11:00 PM
Rating: