Loading...

Juma Abdul amesaini Azam FC?


BEKI wa kulia wa Yanga, Juma Abdul, inadaiwa ameiacha timu yake hiyo kwenye mataa baada ya kuingia mkataba mpya na Azam ambao wameamua kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Abdul ni beki bora kwa sasa wa kulia kutokana na soka analoonyesha, huku akiwa anasifika katika kupandisha mashambulizi, lakini ni hatari sana katika upigaji wa krosi za ‘ndizi’.

Ukiachana na sifa hizo, Abdul amechangia mabao mengi katika kikosi cha Yanga msimu uliopita kutokana na krosi zake hizo maridadi.

Azam wameamua kumsajili Abdul baada ya kuondoka kwa beki wao wa kulia, Shomari Kapombe aliyesajiliwa na Simba jana na kuwaacha kwenye mataa dakika za lala salama.

Tetesi hizo za Abdul kusajiliwa na Azam zilianza pale beki huyo alipotumia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika: “Thanks God deal done.” Ujumbe wake huo ulizua taharuki kwa mashabiki wake na wa Yanga kabla ya kuzagaa tetesi kuwa ametua Azam.

Licha ya kugoma kupokea simu yake kueleza ukweli wa jambo hilo, habari za za uhakika kutoka ndani zinasema kuwa beki huyo amemalizana na Azam na sasa ni mchezaji wao halali.

Wakati huo huo, Yanga imeelezwa kuwa imemsainisha mkataba wa awali wa miaka miwili kipa wa African Lyon, Youthe Rostand, wenye thamani ya Sh milioni 20, huku akitarajiwa kulipwa mshahara wa Dola za Marekani 1200 (sawa na Sh mil 2.6) na tayari amepewa Dola 1000 (sawa na Sh mil 2.1).

Source: Bingwa
Juma Abdul amesaini Azam FC? Juma Abdul amesaini Azam FC? Reviewed by Zero Degree on 6/13/2017 03:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.