Loading...

AJIRA: Mamlaka ya Mapato Tanzania [TRA] imetangaza nafasi 400 za kazi


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza ajira 400 ikiwamo zile zinazohusu maofisa forodha, maofisa kodi na wachambuzi biashara.

Tangazo lililotolewa jana na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, limewataka Watanzania wenye sifa kutuma maombi yao kabla ya Julai 17 mwaka huu.

Nafasi nyingine zilizotangazwa ni zile zinazohusu rasilimali watu, wasimamizi wa mifumo ya mawasiliano, wanasheria na wahasibu.

Tangazo hilo limesisitiza kuwa wale wanaohisi kuwa na mahitaji maalumu wanapaswa kujieleza kwenye barua zao ambazo zinawezwa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza.

Waombaji wameelekezwa kutuma maombi yao kupitia mtandao wa portal.ajira.go.tz au kutembelea mtandao wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma bofya kiunganishi hiki.
AJIRA: Mamlaka ya Mapato Tanzania [TRA] imetangaza nafasi 400 za kazi AJIRA: Mamlaka ya Mapato Tanzania [TRA] imetangaza nafasi 400 za kazi Reviewed by Zero Degree on 7/04/2017 11:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.