Loading...

Bailey aongezewa marufuku ya mechi nyingine 2


Beki wa Manchester United Eric Bailey amepewa marufuku ya mechi tatu baada ya kupewa kadi nyekundu dhidi ya Celta Vigo katika ligi ya Yuropa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipewa kadi nyekundu katika nusu fainali ya mwezi Mei tarehe 11 na kukosa fainali dhidi ya Ajax, ambayo United ilishinda 2-0.

Hata hivyo marufuku hiyo sasa imeongezwa na itashirikisha mechi mbili.

Bailey atakosa mechi ya kombe la Supercup dhidi ya Real Madrid tarehe 8 mwezi Agosti na mechi ya United katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Kesi ya mchezaji huyo wa Ivory Coast haiwezi kumwezesha kukata rufaa kwa sababu shirikisho la soka Ulaya haliwezi kubadilisha uamuzi wowote isipokuwa ule ambao ulifanywa kimakosa.
Bailey aongezewa marufuku ya mechi nyingine 2 Bailey aongezewa marufuku ya mechi nyingine 2 Reviewed by Zero Degree on 7/25/2017 08:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.