Loading...

Bomu lauwa watu wiwili na kujeruhi mmoja Geita.


Watu wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu lililookotwa na watoto wakidhania kuwa ni chuma chakavu.

Waliofariki dunia ni William Jija mwenye umri wa miaka 35 na Denis Faida mwenye umri wa miaka 5 shuhuda wa tukio hilo amesema bomu liliokotwa na watoto karibu na makazi ya watu ambapo walilipeleka nyumbani kwao wakitarajia kuuza kama chuma chakavu.

Sibomana Mseke ni mshauri wa mgambo wilaya ya Geita na mkuu wa wilaya ya Geita amewataka wananchi kutoa taarifa haraka katika ofisi za vijiji na kata pale wataapoona vitu vinavyotia mashaka.

Hali ya majeruhi inaendelea vizuri na amehamishiwa hospitali ya mkoa geita kwa uchunguzi zaidi.

Source: ITV
Bomu lauwa watu wiwili na kujeruhi mmoja Geita. Bomu lauwa watu wiwili na kujeruhi mmoja Geita. Reviewed by Zero Degree on 7/02/2017 01:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.