Chelsea yataja dau la kwanza kwa anayehitaji kumnunua Diego Costa
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Chelsea wanataka kiasi cha paundi milioni 60 kama ada ya uhamisho ili kumuachia mshambuliaji huyo.
Besiktas wana matamanio makubwa ya kumsajili Costa walau hata kwa sehemu ya muda wa msimu mmoja na hapo kiasi chote cha fedha kingekuwa kama kimepotea ukilinganisha na jinsi Chelsea na Atletico walivyokuwa wamekwisha zungumza.
Atletico wamefungiwa na FIFA kufanya usajili wa wachezaji wapya hadi mwakani. Hata kama wangefanikiwa kukamilisha dili hilo, Costa asingeitumikia Atletico hadi January.
Pia imeripotiwa kwamba, Klabu inayoshiriki Ligi kuu ya China wangemchukua Costa, lakini wanasikitishwa na kitendo chake kutamka mbele ya vyombo vya habari kuhusu ishu ya kwamba ameshafanya mazungumzo na Klabu hiyo ilikuwa ni habari ya uongo na sio ya ukweli.
Ripoti nyingine zinadai kwamba, Chelsea watajaribu kuchekechua hata kama ni kutafuta dili zuri la mkopo kwa straika Diego Costa.
'The Times' wanadai Antonio Conte alikutana na mmiliki wa Klabu ya Chelsea, Roman Abramovich wiki iliyopita kujadili mipango yao ya msimu ujao.
Mfanyabiashara huyo wa Urusi alikubaliana na mwami huyo wa zamani wa Juventus kwamba Costa ataondoka Magharibi ya Londoni katika majira haya ya joto.
Inasemekana kwamba Chelsea wana nia madhubuti ya kumtafuta mteja wa kumnunua straika huyu mzaliwa wa taifa la Brazili.
Hata hivyo, watakusudia kuhamia kwenye dili la kumtoa kwa mkopo kwa nusu ya kwanza ya msimu endapo hatatokea wa kumnunua.
Wakati huo huo, Chelsea wakiwa kwenye kuwinda saini ya Alex Sandro kama ambavyo imeripotiwa, Conte amepata chaguo jingine na lenye thamani nzuri zaidi.
Chelsea yataja dau la kwanza kwa anayehitaji kumnunua Diego Costa
Reviewed by Zero Degree
on
7/09/2017 11:31:00 AM
Rating: