Loading...

Federer ametwaa taji la michuano ya Wimbledon


Mchezaji namba tano kwa ubora wa mchezo tenesi Roger Federer ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji la michuano ya Wimbledon, kwa mara nane.


Federer ametwaa taji hilo la Grand Slam baada ya kumshinda mpinzani wake Marin Cilic, kwa jumla ya seti tatu.

Katika seti ya kwanza bingwa huyu wa kihistoria alishinda kwa 6-3, kisha akashinda kwa 6-1 na kumaliza kwa 6-4, katika mchezo ulichezwa kwa muda wa saa moja na na dakika 41.

Hili ni taji la 19 la Grand Slam, kwa mchezaji huyu raia wa Switzerland, na kuwa mchezaji mkubwa zaidi kutwaa mataji yote ya michuano ya wazi ya England.
Federer ametwaa taji la michuano ya Wimbledon Federer ametwaa taji la michuano ya Wimbledon Reviewed by Zero Degree on 7/17/2017 10:12:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.