Loading...

Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 12


MTUNZI: MC Short Charles Gwimo

Ilipoishia.........Alinilamba lamba eneo la sikio langu huku akininong’oneza kwa maneno haya, “Jana uliamua kunibania kwa kutokuja kwenye disko lakini nakuapia kuwa, nitakutafuta popote utakapokuwa wakati wa likizo ili niifanikishe adhima ya moyo wangu. Tumeumbwa ili tupeane vya bayana na tafsida ila wewe unajifanya kuwa mgumu. Ulikabidhiwa hiyo chururu yako kwa malengo ya kuchurururisha zaidi ya mkojo ila wewe hautaki kuitimizia haja yake muhimu hapa duniani, hebu yatimize malengo hayo usije ukafukiwa nayo ikawa zaidi ya mchwa na mafunza.” Aliniachia kwa busu ambalo nilihisi kuwa ngoma ya sikio langu imepasuka. Hayo ni miongoni mwa mabusu ambayo hubusiwa watu wenye nyota za kupendwa na hawa viumbe wa kike kama kina sisi.

Endelea nayo: Maagano yalifanyika kwa hali ya usalama kabisa huku wengine wakibubujikwa na machozi ya “Kuagana ni huzuni, heri ingekuwa kesho”. Dereva alikanyaga mafuta akiashiria kuwa safari i tayari akituacha tukiwa tumeyatoa macho kodo mithili ya mjusi aliyebanwa kwenye mlango na wengine wakiwa vinywa wazi kama mtoto anayesumbuliwa na kwikwi. Ukimya ulitawala kwa kiasi kikubwa sana kana kwamba tuliishi na hao dada zetu kwa zaidi ya mwaka mmoja na ushei. Tulianza kutawanyika kwa mtawanyiko usio rasmi kwa kila mmoja kufuata uelekeo anaoufahamu. Nilitamani nielekee kanisani kufanya kitubio kwa maovu niliyoyatenda ili Mwenyezi Mungu anifanyie maghufira lakini upande mwingine moyo wangu ulinigomea kwa kujiona si madhambi kwa vitendo nilivyofanya jana yake bali niliendana na maandiko matakatifu yasemayo, zaeni muongezeke mkaijaze dunia……. Sasa dunia itajaaje kama hatukuanza mazoezi ya kuongeza watu mapema? Niliyapuuzia mawazo ya kwenda kanisani na hapo ndipo nilipogundua kuwa kwenye dhambi shetani huwa na ushawishi mkubwa kwa waja wa Mungu kuliko maelezo. Kiufupi ni kwamba asubuhi hiyo tuligawanyika kama ifuatavyo, wapo walioenda kanisani, wapo wailoelekea bwenini kujipumzisha na wapo walioingia mitaani kumangamanga ili waimalizie jumapili salama kabla ya kengele ya ukaguzi kwa wanafunzi ipigwayo saa kumi na moja kamili jioni.


**********

Nilielekea kujipumzisha chini ya kivuli cha mti wa mlimao uliokuwa pembeni ya bweni letu lengo ikiwa ni kumsubiri rafiki yangu kipenzi ambaye hatukuonana tena tangu usiku ule wa kwenye disko. Mapumziko yangu chini ya mti ule wa mlimao yaliambatana na usomaji wa simulizi ya “NEEMA IKIZIDI” iliyowahi kutamba kwenye mtandao wa facebook kwa tambo za uhakika. Nikiwa katika muendelezo wa kuperuzi simulizi hiyo, niligutushwa na sauti ya mkwaruzo mithili ya chura dume aliyenogewa na penzi kwenye maji yaliyotuama. “Oyaa! Man, niaje mwanangu?” Nilipotazama nyuma nilikutana uso kwa uso na mzee wa totozi akiwa na tabasamu lililoenea uso mzima kama vile mtu aliyejishindia mchezo wa “NASIBU” kwa kujinyakulia bingo nene. Nilisimama kisha tukapeana salamu kwa mtindo wa kibega kwa bega kisha tukatulia kwenye benchi letu tayari kwa kulishana simulizi za uongo na kweli ili kila mmoja ajione kijogoo kwa mwenzake kwa matukio yaliyofanyika usiku wa disko na baada ya disko. Mood alinisimulia namna alivyolisakata rumba na watoto wa kishua kwa kuwabadilisha kama vile shuka chafu na chawa. Alinielezea jinsi alivyopagawishwa na Fety kwenye ‘blues’ la “The End of the Road” kwani ghashi huyo hakumpa hata chembe ya nafasi ili akajirushe na mali mpya kutoka Kibondo. Pia alinisimulia jinsi Fety aliavyomfikisha pabaya kitendo kilichowafanya waukimbie ukumbi wa disko na kuelekea viwanja vya malavidavi kuibenjua amri ya sita ya Mwenyezi Mungu waliyosomewa wana wa Israel maeneo ya mlima Sinai na kiongozi wao aitwaye Musa. Mood alijisifia kwa mengi huku mimi nikijifanya mtoto mwema ambaye sikufanikiwa kufanya jambo lolote kumbe nilikuwa nikipulizia pafyumu kenye kinyesi.

***********

Mood alinielezea jinsi alivyolifaidi penzi la Fety kwa kupika na kujipakulia huku ghashi huyo akimuonyesha ufundi mubashara wa mapenzi kutoka nyumbani kwao Tanga kunakosadikiwa kuzaliwa kwa mapenzi yaliyokuja kufia Bukoba. Mtindo uliomuacha hoi ni ule wa “Reebook Pump Style” uliomfanya ahisi kuwa kiuno chake kimepata mteguko. Aliendelea kunimegea habari moto moto za kimapenzi zilizousisimua mwili wangu ingawa nilijikaza kisabuni ili Mood asinihisi na nisije kumpotezea uelekeo wa Simulizi yake. Alipoweka kituo cha simulizi yake, sikusita kumsifia kinafiki kwa kumbatiza jina jipya la “KISUKA” yaani jembe la ukweli katika tasnia ya kuwapa burudani za kikubwa watoto wa kike. Nilimjaza upepo kichwani ili ajiweke kwenye kundi namba moja, asijue kuwa simulizi zake nyingine zilinitia kichefuchefu kwa kujisifia ujinga ingawa na mimi tayari nimeshauvaa ujinga huo pasina kutegemea tena kwa kuandika historia ya kukizindua kizinda cha Shamia bila ganzi yoyote. Sikupenda kumuweka wazi Mood kwa kitendo nilichomfanyia Shamia kwa kuepuka fedheha kwani tokea awali nilikuwa ni mtoto niliyekulia kwenye maadili ya kimungu kwa mujibu wa imani yangu. Nikiwa bado naendelea kumminia sifa za kinafiki, Mood alinikata maneno kwa kunitolea malalamishi kutoka kwa Fety, eti kwanini nilimpotezea Fauzia kwa kutoonekana kwenye disko ilihali yeye alikuja ukumbini kunifuata. Sikuwa na majibu ya moja kwa moja zaidi ya kujichekesha kama Malaya aliyekuwa mawindoni aliyebahatisha buzi bwege. Malalamiko hayo yalihitimishwa kwa Mood kunieleza, Fety na Fey wanatusubiria kwa hamu mchana wa siku hiyo maeneo ya bandari ndogo ya Kibirizi kwa ajili ya maongezi zaidi.

====>>Itaendelea Ijumaa...


Usiikose SEHEMU YA 13>>> ya Riwaya hii ifikapo Ijumaa ya wiki hii, na utaipata hapa Zero Degree pekee.
Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 12 Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 12 Reviewed by Zero Degree on 7/10/2017 02:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.