Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 17
Ilipoishia.........Tuliingia kulala huku tafakuri yangu ikiwa kinyume na kile kilichonisababisha kuwa pale shuleni. Nikiwa kitandani mwangu, mawazo yalinichukua kwa kunitembeza kona mbalimbali za mahaba kwa kunikutanisha na vimwana mbalimbali ambao wengine kwangu niliwaona kama michoro ya kubuni na wengine sikuamini kama wapo kwenye dunia hii ya Mola. Usingizi ulinipitia bila aina yoyote ya njozi mpaka pale niliposhtuliwa na kelele za wanafunzi wenzangu waliokuwa kwenye harakati za kuelekea katika maeneo yao ya kazi, na hapo ndipo nilipogundua kuwa siku niliyokuwa nikijivunia kuiita leo imebadilika jina na kuitwa jana na leo yangu imekuwa Jumatatu.
Endelea nayo: Jumatatu ya mwanzo wa wiki ya masomo haikuwa ya furaha kwangu, jambo ambalo kila mwanafunzi aliweza kulibaini juu yangu. Nilijaribu kuivuta furaha ili nisionekane mpweke lakini uso ulibakia kama ulivyo kwa kusongwa na makunyanzi mithili ya kikongwe wa miaka hamsini au sitini aishiye katika mazingira magumu. Walimu waliingia kwa mfululizo kama ratiba inavyowaongoza huku kila mmoja akijaribu kwenda na silabasi au muhtasari wa somo lake ili aukamilishe haraka iwezekanavyo na kutuacha tuendelee na maandalizi yetu ya mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza. Nilishinda nimejiinamia darasani huku nimeifumbata mikono yangu kwenye mashavu kana kwamba ni mwanamkiwa aliyewakumbuka wazazi wake ambao hakuwahi hata kuziona sura zao tangu azaliwe. Machozi yalinilenga lenga hasa pale kumbukumbu ziliponirudisha kwenye uovu nilioufanya kwenye ukaribisho wetu wa vijana wa kidato cha kwanza. Moyoni niliwaza mengi sana ukiwemo ugonjwa hatari wa UKIMWI kwani katika kufanya yote ya uzinzi kwa Shamia na Fauzia sikutumia zana yoyote ile zaidi ya kucheza mechi zote nikiwa peku peku.
Kumbukumbu ilianza kunirudisha miaka ya themanini na tisa nilipomshuhudia kwa mara ya kwanza mgonjwa aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Ukimwi na kuamua kujiweka wazi wazi kwa kujitangaza kupitia mikanda ya video. Huyu hakuwa mwingine bali ni aliyekuwa mwanamuziki nchini Uganda, Fili Bongole Lutaaya. Nilipofikia hatua ya kumkumbuka mwanamuziki huyo, machozi yalinimwagika pwaaa! Huku nikivuta mafua kama vile nimepaliwa na moshi wa bangi uliochanganyika na vumbi la ugoro.
Niligutushwa na mwalimu wa kipindi cha saa saba, yaani kipindi cha mwisho kwa kuingia darasani ili amalizie kipengele cha mwisho kihusianacho na viumbe hai katika somo lake la Elimu ya viumbe hai. Nilijinyoosha kichovu ili niyaweke maungo sawa kwa kwenda sambamba na kipindi chake. Mwalimu Linda alitokea kunipenda na kunishikilia kama vile mdogo wake wa kuzaliwa tumbo moja. Mwalimu huyo Kigori, alikuwa ni mmoja wa ajira mpya aliyepangiwa kwenye shule yetu. Shule iliyokuwa na walimu wa kiume kuminatisa na mmoja wa kike mama mtu mzima ambaye ndiye alikuwa makamu mkuu wa shule.
Inasemekana ujio wa mwalimu Linda hapo shuleni kwetu, uliweza kuzua tafrani kubwa baina ya walimu ofisini. Kuna wale waliorusha ndoano zao na samaki akakwepa chambo na wengine chambo akiliwa upande upande na samaki akaishia. Kuna wale waliojitangazia kuwa walishakubaliwa kumbe ni mbwembwe tu. Hakika mwalimu Linda alikuwa na sifa zote za kuwagombanisha wanaume wote wasiojielewa katika suala la mapenzi. Madam Linda alikifundisha kipindi chake huku tukiwa kimya kwa usikivu wa kukipenda kipindi ingawa wengine walikaa kimya kwa kuogopa kuuliza maswali kwa kutoijua lugha husika au uoga.
Kipindi kilivyomalizika, Madam Linda aliniomba nimfuate ofisini kwake ili akanijenge kisaikolojia zaidi kwani aliniona kama vile kuna kitu kimenisibu kutokana na hali aliyonikuta nayo darasani kabla hajaanza kipindi chake. Niliambatana naye hadi ofisini kwake kisha tukakaa. Akaanza kwa kunihoji kama ifuatavyo, “Mdogo wangu David, ni jambo gani lilokusibu mpaka kuonekana uhali mbaya kifikra namna hiyo?” “Ninapokutazama, hauko sawa kabisa, jambo ambalo limenitia shaka hata mimi dada yako wa hiari. Hebu nieleze ni magumu gani uliyokumbana nayo yanayokufanya upoteze furaha yako hapa shuleni.” “Kumbuka, mimi ni mwalimu wako na mtu pekee niliyejitolea kuwa dada yako wa hiari kwa hiari yangu mwenyewe. Sasa, ninakuomba uwe muwazi kuniambia yale yote yanayokusibu ili niweze kuyatafutia ufumbuzi wa kina na Amani ya moyo wako irudie pale pale kama awali.”
Kwa muda wote aliokuwa akinihoji yaliyonisibu ni yapi, mkono wake ulikuwa ukinipapasa maeneo mbalimbali ya mwili wangu kama vile mama ambembelezaye mwanaye ili alale. Mpapaso huo ulinifanya nipoteze mawasiliano ya mada husika kwa kujibu kinyume na kile ambacho sikutegemea kukitoa moyoni. Inasemekana nilimjibu kama hivi, “Mpenzi Fauzia ninakuomba unipunguzie uchokozi kwa kunitomasa tomasa kwenye jua hili la mchana, na kuomba uniache kwa leo tu, siku mitihani ikiisha ntakutimizia kile ukitakacho……” Nilishangazwa na swali zito kutoka kwa Madam Linda, “David! Fauzia ni nani na anataka nini kutoka kwako, mbona umemuahidi kumtimizia kitu fulani utakapomaliza mitihani yako?” Swali hilo lilinifanya nikose Amani ya moyo baada ya kugundua kuwa mahali pale si ufukwe wa kibirizi kama mawazo yalivyonituma bali nipo ofisini kwa madam Linda na siri inayoutesa moyo wangu nimeianika juani.
Nilipochelewa kumjibu, madam huyo aling’aka kwa hasira, “Hivi wewe David umekuja hapa shuleni kuwawazia hao vinuka mkojo wako kina Fauzia au umekuja kusoma?” Wazazi wako wako huko kijijini wanashindia mihogo kwa maji ya kunywa wewe unakuja kuleta za kuleta kwa kushindwa kusoma vizuri, sasa utazitambua mbivu mbichi na mbovu dawa yake umejichemshia mwenyewe.” Nilianza kutetemeka mithili ya mwanaume aliyebanwa na ugonjwa wa ngiri huku matone ya mkojo yakijitoa kama bomba la maji lililotoboka.
Nilimpigia magoti madam ili anisamehe kwa kunitunzia siri hiyo ambayo nilimuapia kwa majina yote ya Mwenyezi Mungu kutoyarudia. Madam alipunguza hasira kisha akaniambia nisimame baada ya kupiga magoti. Nilisimama kisha akaniambia, “David, ujue wewe kijana mwenye maumbile mazuri na kwa masomo uko vizuri kwa ujumla, hautakiwi kujichanganya na makundi mabaya yatayokuharibia kesho yako……..kwa leo nitakuadhibu viboko vitatu tu kisha utaniandikia barua ya kukiri kosa lako.”
Niliandika barua ya kukiri makosa yangu kisha nikamkabidhi barua zile mbazo aliziweka kwenye mtoto wa kabati. Kabla hajaziweka mle ndani, alizidondosha kwa makusudi kisha akaomba nimuokotee. Nilipotupa jicho mbele yangu wakati naziokota barua zile, lahaula! Nilikutana na kioja cha karne cha kumuona Linda aliyemsababisha madamu kuitwa Linda. Hapa namaanisha hakuwa amevaa nguo ya ndani zaidi ya kukiachia kitumbua chake nje ya kibali huku eneo lote likiwa pee mithili ya karatasi jeupe.
*******
*******
*******
*******
*******
*******
*******
*******
Usiikose SEHEMU YA 18>>> ya Riwaya hii ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo, na utaipata hapa Zero Degree pekee.
Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 17
Reviewed by Zero Degree
on
7/28/2017 09:47:00 AM
Rating: