Loading...

Kuhusu ishu ya Arsenal na Thomas Lemar wa Monaco, ..hivi ndivyo ilivyo hadi muda huu


Arsenal wanaamini kwamba huenda wakapoteza nafasi ya kumnunua mchezaji ambaye wamekuwa wakimtafuta sana, Thomas Lemar wa klabu ya Monaco.

Gunners bado wanatia juhudi kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wa umri wa miaka 21 lakini sasa kumeibuka wasiwasi kwamba mabingwa hao wa Ufaransa huenda wasikubali kumuuza.

Hii ni baada ya Monaco kuwauzia Chelsea kiungo Tiemoue Bakayoko.

Mchezaji wao mwingine Benjamin Mendy anatarajiwa pia kuwaaga, jambo ambalo linaifanya vigumu kwao kumuuza Lemar.

Hayo yakijiri, Arsenal wamesalia kufanya kila wawezalo kumzuia Alexis Sanchez kuondoka.

Mchezaji huyo wa Chile anaingia mwaka wake wa mwisho kwenye mkataba wake wa sasa katika kalbu hiyo na anadaiwa kutaka kuondoka, lakini Gunners wanataka kumkomalia asalie Emirates. Alikuwa mfungaji bora wao msimu uliopita.

Monaco walimuuza Bakayoko kwa Chelsea kwa paundi milioni 40, naye beki wa kushoto Mendy anahusishwa na kuhamia Manchester City.

Kuna tetesi
 pia kwamba mshambuliaji wao Kylian Mbappe, 18, ambaye pia anatafutwa na Arsenal na Real Madrid anaweza kuondoka.

Arsenal kipindi hiki wamemnunua mshambuliaji Alexandre Lacazette kutoka Lyon kwa £46.5m ambayo ni rekodi kubwa kwao.

Walimchukua pia beki wa kushoto Sead Kolasinac kutoka Schalke bila kulipa ada yoyote baada ya yeye kuwa amemaliza kuutumikia mkataba wake.
Kuhusu ishu ya Arsenal na Thomas Lemar wa Monaco, ..hivi ndivyo ilivyo hadi muda huu Kuhusu ishu ya Arsenal na Thomas Lemar wa Monaco, ..hivi ndivyo ilivyo hadi muda huu Reviewed by Zero Degree on 7/17/2017 12:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.