Loading...

Lipumba atangaza kuwavua uanachama wabunge wa CUF


Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho.

Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam, kwa makosa kama hayo.

Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo leo Jumatatu, Julai 24 wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam.

"Leo asubuhi tumewasilisha nyaraka za hatua hizi kwa Spika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa hatua zaidi," amesema Profesa Lipumba.

Amesema wabunge hao wanane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na Chadema kumwondoa yeye madarakani.
Lipumba atangaza kuwavua uanachama wabunge wa CUF Lipumba atangaza kuwavua uanachama wabunge wa CUF Reviewed by Zero Degree on 7/25/2017 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.