Loading...

Majambazi 6 wameuawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza.


Watu sita wanaoaminika kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi katika eneo la Kwa Magila Jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Bwana AHMED MSANGI amesema watu hao ambao wanadaiwa kuwa ni wahalifu walikaidi kukamatwa na kuanza kuwatupia risasi askari Polisi ili wasikamatwe.

Amesema Jeshi la Polisi lilikuwa likiwafuatilia wahalifu hao baada ya kupata taarifa kutoka wasamaria wema na kwamba wawili mmoja au wawili inadaiwa walikimbia kutoka Mkoa wa Pwani.

Kamanda MSANGI amesema taarifa za kiintelejensia zinasema watu hao walikuwa wakijipanga kutengeneza vikundi vya kufanya uhalifu Mkoani Mwanza.

Amesema baada ya kumkamata mmoja wao aliwapeleka kwa wenzake ambao walipofika eneo linalohusika walianza kuwatupia risasi Polisi na katika majibizano ya risasi wahalifu hao sita wameuawa.
Majambazi 6 wameuawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza. Majambazi 6 wameuawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi Jijini Mwanza. Reviewed by Zero Degree on 7/08/2017 08:34:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.