Monaco yatinga FIFA kuvishtaki vilabu vilivyofanya mazungumzo na Kylian Mbappe kinyume na sheria
Mabingwa hao wa Ufaransa wametoa kauli nzito leo Alhamisi baada ya kuwa wamemuuza Timoue Bakayoko kwa Chelsea na Bernado Silva kwenda Manchester City na wakati huo huo Benjamin Fabiano pamoja na Fabinho wakiwindwa na klabu kubwa za Ulaya.
“AS Monaco wanatoa taarifa hii ya malalamiko kwamba baadhi ya klabu kubwa za Ulaya zimekiuka utaratibu kwa kufanya mazungumzo na Kylian Mbappe bila ruhusa yao. Monaco wanataka kuzikumbusha klabu hizo kwamba vitendo kama hivyo viko kinyume na kifungu namba 211 kwenye sheria za Ligi ya Ufaransa (French Football League) na kifungu 18.3 cha sheria ya mstakabali mzima wa mchezaji na uhamisho wake ya FIFA.
“Kuweka ukomo wa matukio kama hayo, AS Monaco wanaamua kuiomba 'French Football League' (Ligue de Football Professionnel) na FIFA kuziwajibisha klabu hizo kwa kitendo hicho cha uvunjaji wa sheria.”
Ripoti zinaeleza kwamba Paris Saint-Germain na Manchester City ni miongoni mwa klabu zilizoshitakiwa FIFA.
Southampton walipatwa na tukio kama hilo katika majira haya ya joto, walitoa malalmiko yao kwa kitendo cha Liverpool kilichofanywa kwa beki wao nyota na nahodha wa klabu, Virgil Van Dijk. Liverpool waliishia kuomba msamaha mbele ya halaiki na kusema kwamba wataachana kabisa na mchezaji huyo.
Maamuzi ndiyo yanayosubiliwa, na inasubiliwa upatikane upande wenye hatia tu kwa kutofuata utaratibu sahihi.
Monaco yatinga FIFA kuvishtaki vilabu vilivyofanya mazungumzo na Kylian Mbappe kinyume na sheria
Reviewed by Zero Degree
on
7/20/2017 08:04:00 PM
Rating: