Loading...

Ofisi ya Taifa ya Takwimu yatangaza nafasi 450 za kazi


Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inawatangazia watanzania wenye sifa kuomba kazi ya muda ya udadisi au ukusanyaji wa takwimu nafasi 450 kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa mwaka 2017/18 (Household Budget Survey) utakaofanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara.

Utafiti huu unahitaji mwombaji atoke kwenye eneo ambalo utafiti unafanyika na awe tayari kufanya kazi kwa kipindi chote cha miezi 12. Sifa za mwombaji zinazohitajika pamoja na maeneo yaliyochaguliwa kwa ajili ya utafiti huu yameanishwa kwenye tangazo la kazi ambalo linapatikana kwenye kila Ofisi ya Mkoa ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Barua ya maombi ya kazi itumwe kwenye Ofisi ya NBS ya Mkoa ambako unaishi.

Maombi yanatakiwa yatumwe kabla ya tarehe 12 Agosti, 2017

ZINGATIA
  • Tangazo hili linapatikana kupitia www.nbs.go.tz pamoja na www.eastc.ac.tz
  • Wale watakaochaguliwa kwa ajili ya usaili ndio watakaoitwa. NBS haitahusika na gharama za kuja kwenye usaili huu.
IMETOLEWA NA
MKURUGENZI MKUU
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
27 Julai, 2017
Ofisi ya Taifa ya Takwimu yatangaza nafasi 450 za kazi Ofisi ya Taifa ya Takwimu yatangaza nafasi 450 za kazi Reviewed by Zero Degree on 7/30/2017 07:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.