Loading...

Rais azuia mikopo

Rais Yoweri Museveni wa Uganda
Rais Yoweri Museveni wa Uganda, amemuagiza Spika wa Bunge, Rebecca Kadaga, kuhakikisha kwamba, masuala yote yanayohusu mikopo ya serikali yanapita kwake kwa ajili ya kuidhinishwa kabla ya kuwasilishwa bungeni.

Katika barua yake kwa Spika iliyosomwa bungeni jana, Rais Museveni ameagiza mikopo 11 iliyoombwa na serikali ambayo inajadiliwa na wabunge isitishwe kwa maelezo kwamba haina faida kwa uchumi wa taifa hilo.

Aidha, Rais Museveni ameagiza maombi ya mikopo 16 pekee ya serikali ndiyo iidhinishwe na kwamba, sekta za ujenzi wa miundombinu, afya na elimu ndio ipiwe na mikopo hiyo.

Miongoni mwa mikopo ambayo Rais Museven ameipinga ni pamoja na mkopo wa dola milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kuu ya Kampala – Jinja, na dola milioni 100 kutoka Islamic Development Benki kwa ajili ya kupambana na umaskini nchini humo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Matia Kasaijja, deni la ndani na nje la Uganda limefikia dola bilioni 8.7 sawa na 33.8% ya pato la ndani la nchi hiyo.
Rais azuia mikopo Rais azuia mikopo Reviewed by Zero Degree on 7/14/2017 12:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.