Sirro amemteua Kamanda Mpinga kuwa RPC wa Mkoa wa Mbeya
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, MOHAMED MPINGA anakuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,na nafasi yake inachukuliwa na Bwana FORTUNATUS MUSILIM.
Taarifa ya Jeshi la Polisi kwa vyombo vya Habari zinasena aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Bwana DHAHIRI KIDAVASHARI amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Sirro amemteua Kamanda Mpinga kuwa RPC wa Mkoa wa Mbeya
Reviewed by Zero Degree
on
7/13/2017 07:53:00 PM
Rating: