Loading...

Taifa Stars yaibuka mshindi wa 3 katika Michuano ya Kombe la Cosafa


Taifa Stars imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Cosafa baada ya kuichapa Lesotho kwa mikwaju ya penalti.

Stars imeibuka na ushindi wa mikwaju 4-3 dhidi ya Lesotho baada ya dakika 90 za bila kufungana.

Katika michuano hiyo inayopigwa nchini Afrika Kusini, Shiza Kichuya ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga na kukosa.

Hata hivyo baadaye Lesotho walipoteza penalti mbili, moja ikigonga mwamba na nyingine kipa Said Mohamed ‘Nduda’ akikoa moja.

Waliofunga upande wa Stars ni Himid Mao, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Alpha aliyema malizia kazi.
Taifa Stars yaibuka mshindi wa 3 katika Michuano ya Kombe la Cosafa Taifa Stars yaibuka mshindi wa 3 katika Michuano ya Kombe la Cosafa Reviewed by Zero Degree on 7/08/2017 08:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.