Loading...

Zimbabwe ndio mabingwa wapya wa Kombe la Cosafa


Vijana wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, wametawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Cosafa 2017, baada ya kuiadhibu Zambia kwa mbao 3-1 kwenye dimba la Royal Bafokeng mjini Restenburg, Afrika Kusini.

Zimbabwe wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo ikiwa ni mara yao ya tano kwenye mashindano hayo.

Kocha wa timu hiyo, Sunday Chidzambwa amejiwekea rekodi baada ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa taji hilo mara tatu kwenye mashindano hayo ambapo pia aliwahi kuibuka kinara mwaka 2003 na 2009.

Licha ya Kocha wa Zambia, Wedson Nyirenda kufanya mabadiliko kadhaa uwanjani, lakini kikosi chake hakikuweza kufurukuta mbele ya vijana hao wa Zimbabwe na mchezo kumalizika kwa ushindi huo.
Zimbabwe ndio mabingwa wapya wa Kombe la Cosafa Zimbabwe ndio mabingwa wapya wa Kombe la Cosafa Reviewed by Zero Degree on 7/09/2017 08:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.