Loading...

AJALI: Mmoja afariki baada ya Basi kugonga Treni mkoani Morogoro


Mmoja amefariki baada ya basi walilokuwa wamepanda wanafunzi wakienda shule kugonga treni katika eneo la Tanesco mkoani Morogoro, ajali iliyotokea asubuhi ya alhamisi ya Agosti, 24.


Taarifa ya kifo hicho imethibitishwa na Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Frank Jacob.

Hata hivyo katika tukio hilo watu wawili inasemekana wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu.


Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo.
AJALI: Mmoja afariki baada ya Basi kugonga Treni mkoani Morogoro AJALI: Mmoja afariki baada ya Basi kugonga Treni mkoani Morogoro Reviewed by Zero Degree on 8/24/2017 10:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.