Loading...

Barca yagonga mwamba kwa Philippe Coutinho


Liverpool wamekataa ombi la Barcelona la kutaka kumnunua mchezaji raia wa Brazil Philippe Coutinho kwa kima cha pauni milioni 90.

Hili ndilo ombi la pili kutolewa na Barcelona baada ya lile la kwanza la pauni milioni 72 kukataliwa

Liverpool wamesisitiza kuwa Coutinho ambaye alijiunga nao kutoka Inter Milan mwaka 2013 kwa pauni milioni 8.5 hauzwi.

Barcelona walimuuza mshambuliaji wake Neymar kwenda St-Germain kwa kima cha pauni milioni 200 wiki iliyopita.

Coutinho ambaye alifunga mabao 14 msimu uliopita alikaa muda wa wiki sita kutokana na jeraha, alisaini mkataba wa miaka mitano mwezi Januari.
Barca yagonga mwamba kwa Philippe Coutinho Barca yagonga mwamba kwa Philippe Coutinho Reviewed by Zero Degree on 8/10/2017 01:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.